CHALLENGES OF TRANSFORMING A TECHNICAL INSTITUTE INTO A UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY A Valedictory Message to the Mbeya University of Science and Technology (MUST) Let me begin by thanking the appointing authority for the unique opportunity availed to me to serve as Chancellor of the Mbeya University of Science and Technology from April 2014 to December 1018. Furthermore I congratulate, most sincerely, Honourable Pius Msekwa and Honourable Zakia Meghji upon their appointment as Chancellor and Chairperson of Council, respectively. I wish them all the best in their new role as principal overseers of the University. Secondly, this address is meant to provide advice to the incoming leadership of the University based on the limited but exciting time I have had as the founding Chancellor of this young and emerging scientific and technological University. However, I am cautious about this prospect. For how can one offer advice to a veteran of higher educati...
UJUMBE WA TASIHILI (A VALEDICTORY MESSAGE) KWA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST) Naanza kwa kuishukuru Mamlaka ya Uteuzi kwa kuniwezesha kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kuanzia 2014 mpaka 2018. Aidha nawapongeza, Mhe. Pius Msekwa na Mhe. Zakia Meghji, kwa uteuzi wao kuwa Mkuu wa Chuo, na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, mtawalia. Nawatakia kila la heri katika ulezi na usimamizi wa Chuo. Pili, ingawa nauita ushauri, kwa kweli ni ujumbe wa shukrani kwa Mamlaka ya Uteuzi na maelezo mafupi kuhusu uzoefu mdogo nilioupata nikiwa Mkuu wa Chuo Mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST). Kwani nitawezaje kutoa ushauri kwa Mkuu wa Chuo ambaye muda wake mrefu wa utumishi wake kwa Umma amekuwa katika maendeleo ya elimu ya juu, akiwa Makamu Mkuu Mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maana hiyo MUST itafaidika pia kutokana na uzoe...