Kwaheri Mhandisi Ngusa Laurent Izengo 1972 - 2018 Mwaka 2008, niliteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Awali ya hapo nilikuwa Waziri wa Nchi (Ofisi ya Makamu wa Rais) Mazingira, na kabla ya hapo, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi. Moja ya changamoto kubwa ya Waziri awaye yote ni kumpata Katibu wa Waziri ambaye ndiye msaidizi mkuu, mratibu na msimamizi mkuu wa ofisi ya Waziri. Katibu Mkuu wa Wizara ambaye ndiye afisa mtendaji mkuu wa Wizara, akisaidiwa na Mkurugenzi wa Utumishi ndio wanaomsaidia Waziri katika kumpata mmoja wa watumishi waandamizi, kuwa Katibu wa Waziri. Kwa kuwa Katibu wa Waziri anafanya kazi na Waziri, basi anayependekezwa lazima akubalike na Waziri. Katibu ndiye anayepanga ratiba ya kazi ya Waziri. Katibu wa Waziri ndiye anayewaona kwanza wageni wote wa Waziri. Katibu ndiye anayechukua kumbukumbu ya vikao vyote vya Waziri. Katibu wa Waziri ndiye kiungo cha muda wote kati ya Waziri na watendaji wa Wizara. Ingawa K...
Personal Reflections and Narrations